Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

SIKU 6 YA 31

Eliezeri alikuwa amemaliza kutoa habari ya safari yake. Ndipo baba na kaka wa Rebeka wakatambua kuwa huo ni mpango wa Bwana, wala hawakumzuia Rebeka kwenda naye (m.50-51, Labani na Bethueli wakajibu wakasema, Neno hili limetoka kwa Bwana, … Tazama, huyo Rebeka yuko mbele yako, umchukue, ukaende zako awe mke wa mwana wa bwana wako, kama alivyosema Bwana). Rebeka mwenyewe naye alikubali (m.58, Wakamwita Rebeka wakamwuliza, Je! Utakwenda na mtu huyu? Akasema, Nitakwenda)! Na Eliezeri alikumbuka sana agizo la Ibrahimu kwamba Isaka hawezi kwenda kukaa mji wa Nahori, bali mke wake lazima aende Kanaani (m.6-7, Ibrahimu akamwambia [yule mtumishi], Ujihadhari, usimrudishe mwanangu huko)! Kwa hiyo walipotaka abaki kwanza siku kumi hakupendezwa. Akaomba aondoke mara moja. Aliogopa kukawia. Na Isaka akampenda Rebeka (m.67, Rebeka, akawa mkewe, [Isaka] akampenda)! 

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha