Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

SIKU 9 YA 31

Mungu akaithibitisha tena kwa Isaka ahadi aliyompa Ibrahimu (m.3-4, Nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako). Ahadi ya Mungu ilikuwa na sehemu tatu: kupewa nchi ya Kanaani, kupata uzao kwa wingi, na mataifa yote ya dunia kubarikiwa katika uzao wake (unaweza kutazama 12:1-3 na 13:14-18). Ni wazi kwamba utii na imani ya Ibrahimu ikaleta baraka kwa mwanawe (m.5, … katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia. Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu …). Ila ujanja wa Ibrahimu ukamletea matatizo Isaka. Maana akaiga mfano wa baba yake kusema kwamba mke wake ni dada yake ili wasimwue (rudia m.6-11 ukipenda). Je, watoto wako waona mfano gani kwako? 

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha