Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

SIKU 3 YA 31

Sura hii yote inahusu namna Isaka alivyompata mke wake. Ni masimulizi mazuri sana ya kupendeza. Hata katika hatua hii ya maisha ya Ibrahimu Mungu yumo. Tuendelee kujifunza kutokana na imani yake! 1. Kwa sababu ya imani alibarikiwa na Bwana katika vitu vyote (m.1, Bwana alikuwa amembariki Ibrahimu katika vitu vyote). 2. Kwa sababu ya imani alitaka mke wa Isaka awe mcha Mungu (m.3-4, Nitakuapisha kwa Bwana, Mungu wa mbingu, na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke katika binti za Wakanaani ambao nakaa kati yao; bali enenda hata nchi yangu, na kwa jamaa zangu, ukamtwalie mwanangu Isaka mke). 3. Kwa sababu ya imani, lazima Isaka abaki Kanaani, na mke wake ahame aje kwake (m.5-8, Ibrahimu akamwambia [yule mtumishi], Ujihadhari, usimrudishe mwanangu huko. Bwana, Mungu wa mbingu, aliyenitoa katika nyumba ya babangu, … aliniapia akisema, Nitawapa uzao wako nchi hii … yule mwanamke asipokubali kufuatana nawe, basi, utafunguliwa kiapo changu hiki; lakini usimrudishe mwanangu huko.). 4. Kwa sababu ya imani, mpango wa kumwoza Isaka ulifanikiwa sana (m.7, Yeye [Mungu] atampeleka malaika wake mbele yako, nawe utamtwalia mwanangu mke)!

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha