Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021

SIKU 4 YA 31

Maono haya hulenga kuonyesha hukumu ya yule kahaba mkuu (m.1). Ni mfano wa utawala wa mpinga Kristo ambao nguvu yake ni ya kidini hasa. Katika m.5 ametajwa mwanamke aitwaye Mama wa Makahaba, na ukahaba ni uasherati. Lakini pamoja na maana hii ya kawaida, Biblia pia huufananisha na hali ya kumwacha Mungu na kuiabudu miungu. Hali hii ni sawa na kuchukua vyote vizuri ulivyopewa na Mungu, ukajifanyia sanamu za wanaume, ukafanya mambo ya kikahaba juu yake (Eze 16:15-20). Lazima tutambue kwamba uwe uasherati wa kimwili au wa kiroho, makahaba wa namna zote huua! Tunaambiwa hivyo katika m.6 ikiandikwa kwamba huyo mwanamke amelewa kwa damu ya watakatifu. Jiepushe kabisa na vishawishi vyote vinavyotaka kukuvuta mbali na Mungu. Ahadi ya Kristo kwa waaminifu ni taji ya uzima. Bwana wetu Yesu anasema, Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima (Ufu 2:10).

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Desemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Desemba, pamoja na ufafanuzi mfupi wa kukusaidia kuelewa na kutafakari zaidi Neno la Mungu. Katika mpango huu u...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha