Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

SIKU 3 YA 30

Kanisa la Korintho lilikabiliwa na mafundisho ya utamaduni na mapokeo ya Kigiriki. Mafundisho hayo yalitenganisha mwili na roho. Wagiriki hawakuamini juu ya ufufuo wa mwili. Waliona kuwa ufufuo unaihusu roho peke yake na siyo mwili. Walikaza kuwa mwili ni gereza la roho. Roho inatengana na mwili kwa njia ya kifo. Biblia inafundisha kuwa mwili na roho havitenganishwi milele. Kristo katika ufufuo ataifanya miili yetu hii ionekane kwa upya. Ataubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake(Flp 3:21). Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita(Ufu 21:4; ukiwa na nafasi, soma zaidi katika 1 Kor 15:46-58). 

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karib...

More

Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha