Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 09/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

SIKU 7 YA 30

Fungu la maneno haya ni baadhi ya maneno yanayosumbua na hata kuligawanya kundi la wanaomwamini Kristo. Kinacholengwa na mtume Paulo hapa si kujitenga na wasio Wakristo au wasiookoka. La hasha! Hiyo inaeleweka tukisoma aliyoandika sehemu nyingine: Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi. Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia(1 Kor 5:9-10). Watu wengine nawaambia mimi, wala si Bwana, ya kwamba iwapo ndugu mmoja ana mke asiyeamini, na mke huyo anakubali kukaa naye asimwache.Na mwanamke, ambaye ana mume asiyeamini, na mume huyo anakubali kukaa naye, asimwache mumewe(1 Kor 7:12-13). Kinachosemwa hapa ni kututaka Wakristo kutokufungamana na tabia na matendo ya wasiomwamini Kristo. Wakristo tuishi katikati ya wasiomwamini Kristo kwa lengo la kuishuhudia Injili. Kumbuka mwisho wa somo la leo: Basi, wapenzi wangu, kwa kuwa tuna ahadi hizo, na tujitakase nafsi zetu na uchafu wote wa mwili na roho, huku tukitimiza utakatifu katika kumcha Mungu. Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu ye yote, wala kumharibu mtu, wala kumkaramkia mtu(2 Kor 7:1-2). Tujifunze na kuiga mfano wa Yesu Kristo mwenyewe. (Ukiwa na nafasi, soma k.m. Lk 19:1-10).

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 09/2020

Soma Biblia Kila Siku 09/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karib...

More

Nos gustaría agradecer a Soma Biblia por brindar este plan. Para mayor información por favor visite: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha