Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

SIKU 3 YA 30

Ni pendo la namna gani alilotupa Baba (m.1). Mungu hakuuhakikisha upendo wake kwa neno tu, hata alitupa upendo wake kwa njia ya Kristo. Kumbuka mfano wa Mwana mpotevu, jinsi baba yake alivyompa upendo wake. Kuna habari tunazozijua, na kuna habari tusizozijua (m.2). Hizo za mwisho zitaonekana Yesu atakaporudi. Tutamwona katika utukufu wake. Hapa duniani tulimwona kama binadamu. Alikuwa kama sisi ili sisi tupate kumwona kama yeye alivyo katika utukufu wake. Zingatia m.3: Kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.Neno hili kuhusu kujitakasa si amri, bali ni matokeo ya yaliyotangulia kutendeka. Hivyo ni hali halisi ...kama yeye [Yesu]alivyomtakatifu.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Kari...

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha