Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 06/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

SIKU 2 YA 30

Mafuta yale mliyoyapata kwake yanakaa ndani yenu (m.27 na 20). Yesu anapoitwa Kristo, inamaanisha kwamba ni yule Mungu aliyemtia mafuta, yaani, Roho Mtakatifu (ling. Mdo 10:38: Habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye). Sisi tunaomwamini tumepakwa mafuta (Roho Mtakatifu) kutoka kwake, na yeye anatufundisha ukweli. Bila shaka Mtume hapa amekumbuka neno la Yesu katika Yn 16:13: Atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote. Roho Mtakatifu anapopata nafasi mioyoni mwetu, tunatambua kwamba uongo na kweli haupatani. Kwa nguvu ya Neno la Mungu na Roho Mtakatifu uhai wa Wakristo utatunzwa mpaka Kristo atakaporudi.

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 06/2020

Soma Biblia Kila Siku 06/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 1 Yohana, Ayubu na Mathayo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Kari...

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha