Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 5Mfano

Soma Biblia Kila Siku 5

SIKU 2 YA 31

Bwana Yesu aja ([Bwana] apate kuifanya imara mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu, Baba yetu, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu pamoja na watakatifu wake wote; 3:13)! Hivyo Wakristo waonywa waishi maisha maadilifu. Mungu hutaka waumini watakaswe (m.3), kwa hiyo amewapa Roho Mtakatifu (m.8). Maana ya "kutakaswa"ni kutenganishwa na uovu (m.3 na 5f) ili tumtumikie Mungu kwa miili yetu kama chombo (m. 4). Hiyo ni kazi ya Mungu mwenyewe ndani yetu. Kwa hiyo si maisha yetu maadilifu yanayotustahilisha siku ya hukumu. Lakini huyu asiyetaka kutakaswa bali kudumu katika dhambi, humkataa Mungu na kujiweka chini ya hukumu yake (m.8 na 6).

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 5

Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha