Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 5Mfano

Soma Biblia Kila Siku 5

SIKU 1 YA 31

Paulo anajitahidi kuomba awaone tena (usiku na mchana tunapoomba kwa juhudi tupate kuwaona nyuso zenu; 3:10), maana anaona ni Shetani anayemzuia (tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia; 2:18). Upendo ule ambao unamfanya Paulo awaombee (m.12) ni kipaji cha Mungu kinachomiminwa na Roho mioyoni mwa watu wanapopata kuamini. Upendo ni kama tunda la imani linalokua na kujaa tele, hata muumini awe bubujiko la matendo ya upendo (ling. 2 Pet 1:8: Mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo). Pamoja na kuwafaidia wengine wote (m.12), kazi hiyo ya Mungu mioyoni mwa waumini huwaimarisha wenyewe wapate kusimama siku ya Bwana (m. 13). Zingatia Mungu alivyojibu ombi la Paulo: Ndugu, imetupasa kumshukuru Mungu sikuzote kwa ajili yenu, kama ilivyo wajibu, kwa kuwa imani yenu inazidi sana, na upenda wa kila mtu kwenu kwa mwenzake umekuwa mwingi(2 The 1:3)!

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 5

Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha