Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 5Mfano

Soma Biblia Kila Siku 5

SIKU 7 YA 31

Wasiomwamini Yesu hakika hawataokolewa (Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula; 5:3). Lakini si mpango wa Mungu kwao. Hakuwateua kwa ajili ya upotevu wa milele. Maana hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu (m.9; ling. 1 Tim 2:4: Mungu Mwokozi wetu ... hutaka watu  wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli). Twaweza kuwa na uhakika, maana Yesu alikufa kwa ajili yetu (m. 10; zingatia pia Rum 8:32: Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?). Katika m. 10 Paulo anabadilisha mfano. Maana ya "kulala" (m.10) si kulala usingizi wa kiroho kama katika 5:6f, bali "kulala mauti" (4:15). Yaani tuwe hai, tuwe tumekufa, Yesu akija, sote tutaishi pamoja naye milele. Tujengane katika tumaini hili!

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 5

Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha