Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 5Mfano

Soma Biblia Kila Siku 5

SIKU 5 YA 31

Maishani mwetu kuna mapito mengi. Waisraeli waliposafiri kuelekea Yerusalemu, walikumbuka matukio mengi ambayo yalilipata jiji hilo – mambo ambayo hata Wakristo wa siku hizi huweza kuyapata. Je, katika hayo yote tunapaswa kumtumaini nani? Zaburi hutukumbusha kuwa Yerusalemu iliingiliwa na maadui, lakini hawakuruhusiwa kutawala (m.3). Huu ulikuwa ulinzi wa Mungu kwa watu wake. Mwamini wa Mungu ni kama Yerusalemu kwa usalama wake. Tumtumaini Mungu, maana atuokoa na kutupa amani na ulinzi.

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 5

Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha