Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mabadiliko ya Mwana Mpotevu na Kyle IdlemanMfano

Prodigal Son Transformation With Kyle Idleman

SIKU 7 YA 7

“Neema kwa wana wote”

Mwana mkubwa alikasirika baada ya kuona vitendo vya baba yake. Huyu kaka mkubwa anaweza kuwa alifanya kazi kwa bidii na na kutunza mashamba kwa uaminifu, lakini juhudi haikuonekana katika nyumba ya baba yake.


Hakukuwa na uamsho. Hakukuwa na uaminifu. Hakukuwa na hatua.


Ukweli ni kwamba, Hata yeye pia, alikuwa ni mwana mpotevu. Hata yeye pia alikuwa na moyo uliokuwa mbali na baba. Hata yeye alikuwa amepotea lakini hakuliona hilo. Tim Keller anaiweka katika namna hii, “Mwana mbaya alipotea katika ubaya wake, lakini mwana mwema alipotea katika wema wake.”


Labda haujawahi kuwa katika Nchi ya Mbali. Unaweza kuwa na wasifu mzuri sana wa kidini. Labda unafuata sheria zote. Labda umesoma kitabu hiki chote ukifikiria watu wote unaowajua katika Nchi ya Mbali ambao wanahitaji kuisikia. Lakini nashangaa kama wewe ndiye yule ambaye Yesu amekuwa akiongea naye wakati wote.


Kwa bahati nzuri, wakati kaka mkubwa akiwa shambani, baba aliondoka kwenye sherehe na kumwendea. Alimshirikisha mtoto huyo moja kwa moja.


Je! Jambo hili linatuambia nini juu ya Mungu? Mungu anatamani uhusiano na watoto wake. Haijalishi maisha yako yanafanana na ya kaka mkubwa au mdogo.


Hata baada ya uchaguzi wa kufedhehesha wa mtoto mdogo na kuishi bila kujali, baba alimpokea kwa moyo wote kwa kumbusu na kumkumbatia. Na baada ya maneno makali na ukosefu wa heshima wa kaka mkubwa, baba alifafanua jambo hilo mwenyewe kwa upendo. Mkuu wa familia hakuwa na ulazima kamwe wa kujielezea katika nyakati za zamani. Kaya hazikuwa za kidemokrasia; zilikuwa za udikteta. Lakini baba alijibu hasira ya kaka mkubwa kwa ustahimilivu mwema na neema.


Tunatarajia Mungu kuwa baba mwenye hasira anayedai haki, lakini kupitia Yesu, Yeye hutupa upendo na neema wakati tukiwa hatustahili. Hatimaye, hadithi katika Luka 15 haihusu wana wawili ambao si watii. Ni kuhusu Baba anayependa watoto wake bila kikomo.


*Unapokuwa umetenda dhambi, je! Unamuonaje Mungu na kile anachofikiria juu yako? Je! Neema yake isiyo na mwisho na upendo huchocheaje mchakato mzima wa AHA?


Je! Umefurahia mpango huu wa kusoma? Ikiwa ndivyo, ingia kushinda kitabu kamili hapa


siku 6

Kuhusu Mpango huu

Prodigal Son Transformation With Kyle Idleman

Imechukuliwa kutoka kwenye kitabu chake "AHA," ungana na Kyle Idleman anapovumbua mambo 3 yanayoweza kutuleta karibu na Mungu na kubadilisha maisha yetu kabisa. Uko tayari kwa wakati wa Mungu unaobadilisha kila kitu?

Tungependa kumshukuru David C Cook kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.dccpromo.com/aha/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha