Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mabadiliko ya Mwana Mpotevu na Kyle IdlemanMfano

Prodigal Son Transformation With Kyle Idleman

SIKU 1 YA 7

“Mapishi ya AHA”

Mke wangu alikuwa na kitabu cha mapishi nyumbani, zawadi ya harusi yetu. Kinaitwa " Viungo Vitatu vya Kitabu cha Mapishi." Angependa nikwambie kwamba huwa hakitumii kabisa. Anapopika, kuna viungo zaidi ya vitatu vinavyohusika. Ukweli ni kwamba mimi ndiye huwa natumia "Viungo Vitatu vya Kitabu cha Mapishi."


Mara chache sana huwa naruhusiwa jikoni, na kitabu hiki cha mapishi ni mshirika wangu katika mapishi, kwa sababu ukweli, viungo vitatu ni kuhusu uwezo wangu wa kupika. Moja ya mambo ambayo nimejifunza kwa shida ni kwamba napotumia "Viungo Vitatu vya Kitabu cha Mapishi." viungo vyote ni muhimu- hapana, ni vya lazima.


Hii ndiyo hasara ya Viungo Vitatu vya Kitabu cha Mapishi. Huwezi kudanyanya. Ukitumia viungo viwili tuu, mapishi hayawi mazuri.


Ndivyo hivyo kwenye uzoefu wa AHA.


Nimesikiliza uzoefu wa AHA wa mamia- kama si maelfu- ya watu kwa miaka mingi. Nimesoma mabadiliko kadha ya uzoefu wa watu muhimu katika Biblia. Kwa uthabiti mkubwa, AHA siku zote ina viungo vitatu. Kama kiungo kimojawapo kinakosekana, kinaathiri hatua za mabadiliko:


(1) Uamsho wa ghafla (2) Ukweli mchungu (3) Kitendo cha haraka (Awakening, Honesty, Action = AHA)


Kama kuna uamsho na ukweli, lakini hakuna kitendo, kwa hiyo AHA haitokei.


Kama kuna uamsho na kitendo, lakini ukweli umesahaulika, AHA itakuwa ya kitambo tuu.


Lakini neno la Mungu na Roho Mtakatifu vinapoleta hivi vitatu pamoja katika maisha yako, utapata AHA --wakati wa Mungu unaobadilisha kila kitu.


* Uko tayari kwa wakati wa AHA unaokubadilisha? Uko tayari kupitia hatua tatu katika mchakato?


siku 2

Kuhusu Mpango huu

Prodigal Son Transformation With Kyle Idleman

Imechukuliwa kutoka kwenye kitabu chake "AHA," ungana na Kyle Idleman anapovumbua mambo 3 yanayoweza kutuleta karibu na Mungu na kubadilisha maisha yetu kabisa. Uko tayari kwa wakati wa Mungu unaobadilisha kila kitu?

Tungependa kumshukuru David C Cook kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.dccpromo.com/aha/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha