Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mabadiliko ya Mwana Mpotevu na Kyle IdlemanMfano

Prodigal Son Transformation With Kyle Idleman

SIKU 5 YA 7

“UAMINIFU – Uaminifu unaoleta Uponyaji"

Wakristo wengi wanaelewa na kukubali umuhimu wa kuwa mwaminifu, kwao wenyewe na kwa Mungu. Katika 1 Yohana, Biblia inatuambia kwamba tunapoungama dhambi zetu kwa Mungu, Yeye ni mwaminifu na wa haki kutusamehe dhambi zetu na kututakasa na udhalimu wote. Biblia pia inasema kwamba Yesu alichukua adhabu yetu tuliyostahili juu yake alipokufa msalabani. Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zangu, ili kwamba ninapoziungama, Mungu anazisamehe.


Mara nyingi, tunajiambia wenyewe kwamba haitakiwi kuendelea zaidi ya hapo: " Kama ni mwaminifu kwangu mwenyewe na kwa Mungu, hiyo inatosha." Lakini AHA inataka zaidi.


Yakobo 5:16 inazungumza kuungamana dhambi zetu ninyi kwa ninyi " ili muweze kupona." Tunapokuwa waaminifu kwa Mungu kuhusu dhambi zetu, anatusamehe, lakini tunapokuwa waaminifu kwa wengine, tunapata uponyaji.


" Uponyaji" maana yake nini?


Sasa, tabia ya kuungamana dhambi zetu sisi kwa sisi inatufanya kuwajibika na kutusaidia kutiwa moyo tunakokuhitaji kuvunja mduara wa jitihada zetu. Tunapochukua gizani kile tulichokificha na kukileta kikipiga kelele kwenye mwanga, kinapoteza nguvu nyingi juu yetu.


Na uponyaji Yohana anaouzungumza ni zaidi ya halisi kuliko unavyoweza kudhani. Angalia hili: kitabu cha Saikolojia kiitwacho Kukabiliana na Msongo wa mawazo unathibitisha nguvu ya kukiri. Mwandishi anadai kwamba, “watu wanaopendelea kutunza siri wana malalamiko mengi ya mwili na akili, kwa wastani, kuliko watu wasiofanya hivyo... [including] wasiwasi mkubwa, msongo, na dalili za mwili kama maumivu ya mgongo na maumivu ya kichwa… Aibu ya mwanzo ya kuungama mara zote inazidiwa na uhuru unaopata dhidi ya giza la vitu vya siri binafsi."


Mithali 28:13 inachangiza matokeo haya: ““Afichaye dhambi zake hatafanikiwa; Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata.”


* Je, kitendo cha kuungama dhambi zako kwa wengine kumekusaidia huko nyuma? Je, kuna dhambi za siri ambazo umekuwa ukizificha, hutaki kuziweka wazi kwenye mwanga?


siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Prodigal Son Transformation With Kyle Idleman

Imechukuliwa kutoka kwenye kitabu chake "AHA," ungana na Kyle Idleman anapovumbua mambo 3 yanayoweza kutuleta karibu na Mungu na kubadilisha maisha yetu kabisa. Uko tayari kwa wakati wa Mungu unaobadilisha kila kitu?

Tungependa kumshukuru David C Cook kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.dccpromo.com/aha/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha