Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mabadiliko ya Mwana Mpotevu na Kyle IdlemanMfano

Prodigal Son Transformation With Kyle Idleman

SIKU 6 YA 7

“HATUA – Wakati wa kuamka ”

Hatua ndiyo wengi wetu tunakwama. Tunajua nini kinatakiwa kufanyika, tunapanda kwenye mzani, lakini hatuwezi kusogea. Ni jambo moja kuwa na uamsho na hata kuwa wakweli kuhusu tunachohitaji kufanya. Ni kitu kingine kabisa kuchukua hatua. Katika Luka 15:20 tunasoma mstari mfupi ambao ulibadilisha habari ya Mwana Mpotevu. Yesu alisema, "Kwa hiyo kaondoka..."


Alichukua hatua haraka. Alitambua kwamba ni wakati wa kuondoka. Ilikuwa ni muda wa kufanya kitu. Labda kama hadithi yetu inasomeka, "Kwa hiyo alinyanyuka," au "Kwa hiyo alinyanyuka," na hakuna kilichobadilika.


Hapa ndipo AHA hutuchelewesha wengi wetu. Tunamwamko, tunaweza kupata nguvu kuwa waaminifu sana, lakini hatuwezi kufanya chochote tofauti. Maisha yetu mengi yanakwama kati ya uaminifu na kuchukua hatua.


Unaweza kuwa unasoma hili na kufikiria, " Nakubaliana na wewe, lakini sijisikii kufanya chochote juu yake."


Inaweza kuonekana si sawa, au pengine tunakosa msukumo; hata hivyo, ukweli ni kwamba tunahitaji
Mungu hata kama hatujisii. Tunapomtii Mungu pasipo msukumo kufanya hivyo, hisia zetu zitaungana na matendo yetu.


Hebu angalia mpango wako wa mabadiliko unayotaka kuyafanya. Yawezekana umetayarisha orodha, ikiwa kwenye karatasi au kichwani, na unajua ni nini. Panga hatua yako ya kwanza, kama mwana mpotevu alivyofanya alipoamua moyoni mwake, " nitarudi nyumbani kwa baba yangu na kumwambia..." Alijua ni nini anatakiwa kufanya, na alifanya. Tafuta hatua yako ya kwanza na fanyia kazi, ikiwa unataka ama hutaki. Na unaweza kukuta, kwa msaada wa Mungu, hatua ambayo mwanzo ilionekana si halisi inaweza kuthibitishwa.


* Umeamshwa, na mkweli kwako mwenyewe, na hujachukua hatua stahiki? Ni hatua gani ya kwanza unaweza kuchukua kuanza


Andiko

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Prodigal Son Transformation With Kyle Idleman

Imechukuliwa kutoka kwenye kitabu chake "AHA," ungana na Kyle Idleman anapovumbua mambo 3 yanayoweza kutuleta karibu na Mungu na kubadilisha maisha yetu kabisa. Uko tayari kwa wakati wa Mungu unaobadilisha kila kitu?

Tungependa kumshukuru David C Cook kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.dccpromo.com/aha/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha