Zaburi 41:7-9
Zaburi 41:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Wote wanichukiao hunongonezana juu yangu; wananiwazia mabaya ya kunidhuru. Husema: “Maradhi haya yatamuua; hatatoka tena kitandani mwake!” Hata rafiki yangu wa moyoni niliyemwamini, rafiki ambaye alishiriki chakula changu, amegeuka kunishambulia!
Zaburi 41:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wote wanaonichukia wananong'onezana juu yangu, Wananiwazia yaliyo mabaya zaidi. Wanafikiri pigo liualo limemshika, Akalala asiweze kusimama tena. Hata rafiki yangu mwandani niliyemtumaini, Aliyekula pamoja nami, Ameniinulia kisigino chake.
Zaburi 41:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wote wanaonichukia wananinong’ona, Wananiwazia mabaya. Neno la kisirani limemgandama, Na iwapo amelala hatasimama tena. Msiri wangu tena niliyemtumaini, Aliyekula chakula changu, Ameniinulia kisigino chake.
Zaburi 41:7-9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Adui zangu wote hunongʼonezana dhidi yangu, hao huniwazia mabaya sana, wakisema, “Ugonjwa mbaya sana umempata, kamwe hatainuka tena kitandani mwake.” Hata rafiki yangu wa karibu niliyemwamini, yule aliyekula chakula changu ameniinulia kisigino chake.