Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 41

41
Sala ya mgonjwa
(Kwa Mwimbishaji. Zaburi ya Daudi)
1Heri mtu anayewajali maskini;
Mwenyezi-Mungu atamwokoa wakati wa shida.
2Mwenyezi-Mungu atamlinda na kumweka hai,
naye atafanikiwa katika nchi;
Mungu hatamwacha makuchani mwa maadui zake.
3Mwenyezi-Mungu atamsaidia awapo mgonjwa,
atamponya maradhi yake yote.#41:3 atamponya … yote: Maana katika Kiebrania si dhahiri.
4Nami nilisema: “Unifadhili, ee Mwenyezi-Mungu,
unihurumie maana nimekukosea wewe.”
5Madui zangu husema vibaya juu yangu:
“Atakufa lini na jina lake litoweke!”
6Wanitembeleapo husema maneno matupu;
wanakusanya mabaya juu yangu,
na wafikapo nje huwatangazia wengine.
7Wote wanichukiao hunongonezana juu yangu;
wananiwazia mabaya ya kunidhuru.#41:7 wananiwazia … kunidhuru: Au wanawazia mambo mabaya sana.
8Husema: “Maradhi haya yatamuua;
hatatoka tena kitandani mwake!”
9 # Taz Mat 26:23; Marko 14:18; Luka 22:21; Yoh 13:18 Hata rafiki yangu wa moyoni niliyemwamini,
rafiki ambaye alishiriki chakula changu,
amegeuka kunishambulia!
10Ee Mwenyezi-Mungu, unionee huruma!
Unipe nafuu, nami nitawalipiza.
11Hivyo nitajua kwamba unapendezwa nami,
maadui zangu wasipopata fahari juu yangu.
12Wewe umenitegemeza kwani natenda mema;
waniweka mbele yako milele.
13 # Taz Zab 106:48 Asifiwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli,
tangu milele na hata milele!
Amina! Amina!

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 41: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha