Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 41

41
Hakikisho la Msaada wa Mungu na Ombi la Uponyaji
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 # Mit 14:21; Mk 10:21 Heri amkumbukaye mnyonge;
BWANA atamwokoa siku ya taabu.
2BWANA atamlinda na kumhifadhi hai,
Naye atafanikiwa katika nchi;
Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake.
3BWANA atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani.
Katika ugonjwa wake umemtandikia.
4 # Zab 6:2 Nami nalisema, BWANA, unifadhili,
Uniponye roho yangu maana nimekutenda dhambi.
5Adui zangu wananitaja kwa maneno mabaya,
Atakufa lini, jina lake likapotea?
6 # Zab 12:2 Na mmoja wao akija kunitazama asema uongo,
Moyo wake hujikusanyia maovu,
Naye atokapo nje huyanena.
7Wote wanaonichukia wananinong’ona,
Wananiwazia mabaya.
8Neno la kisirani limemgandama,
Na iwapo amelala hatasimama tena.
9 # Mt 26:23; Oba 1:7; Mk 14:18; Lk 22:21; Yn 13:18 Msiri wangu tena niliyemtumaini,
Aliyekula chakula changu,
Ameniinulia kisigino chake.
10Lakini Wewe, BWANA, unifadhili,
Uniinue nipate kuwalipa.
11Kwa neno hili nimejua ya kuwa wapendezwa nami,
Kwa kuwa adui yangu hasimangi kwa kunishinda.
12 # Zab 34:15; Mdo 2:28 Nami katika ukamilifu wangu umenitegemeza,
Umeniweka mbele za uso wako milele.
* * *
13 # Zab 106:48 Na atukuzwe BWANA, Mungu wa Israeli,
Tangu milele hata milele. Amina na Amina.

Iliyochaguliwa sasa

Zab 41: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha