Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mpango wa kupigana Vita vya KirohoMfano

Spiritual Warfare Battle Plan

SIKU 4 YA 5

SIKU YA 4: Chambo ya Uchungu



Nilikuwa nachuja juisi yangu mwenyewe. Mume wangu aliniacha na mtoto wa miaka miwili na lundo la madeni ili aweze kuanza maisha mapya na mwanamke mwenye karibu nusu ya umri wake katika nchi ya ugeni. Nilikuwa nimekasirika na kujawa kisasi. Nilikuwa na uchungu--zaidi ya uchungu-- na sikukumbuka karama ya kupambanua roho kuweza kuiona hii. Nilimchukia, na nilimkasirikia Mungu.



Uchungu unaua. Baada ya muda, uchungu hunajisi roho zetu kufifisha uwezo wetu wa kuhisi uwepo wa Mungu au kusikia sauti yake. Ukimkasirikia Mungu, kuwa muwazi kwake. Mpe hasira yako, na ataigeuza hasira yako kuwa amani na ufunuo mkubwa wa uweza wake kama utamruhusu.



Bwana, nachagua kuwasamehe walioniumiza, nikwaza, nitukana, nitumia kwa dharau, au kunikosea Nisaidie, Bwana, kutambua mbinu za adui kuniteka katika uchungu, kisasi, kutokusamehe. Nisaidie nisiwahesabie makosa walionikosea. Nisaidie kujibu bila moyo wa hukumu ninapoumia. Ponya hisia zangu na fanya upya roho ndani yangu. Katika jina la Yesu. Amen.



    


siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Spiritual Warfare Battle Plan

Kwa haya mafundisho ya nguvu utaelewa kwa kina kuhusu jinsi ya kutengeneza njia ya kumpita adui na kuzuia mpango wake wa kuharibu maisha yako

Tunapenda kushukuru Charisma House kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://bit.ly/spiritualwarfarebattleplan

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha