Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mpango wa kupigana Vita vya KirohoMfano

Spiritual Warfare Battle Plan

SIKU 1 YA 5

SIKU YA KWANZA: Vita dhidi ya Ubaya



Nilipookolewa, nilifikiri nimeishi maisha yangu kutembea pembeni ya maji yaliyosimama na kulala kwenye malisho ya kijani. Nilikuwa sina wazo kuwa na Yesu kama nahodha wa Wokovu wangu ili maanisha kuwa najiandikisha kuwa mwanajeshi wa Mungu.



Toka hapo nimejifunza waamini ni wanajeshi na Yesu hakuja kuleta amani ila alileta upanga. Nimegundua kwamba mimi ni zaidi ya mshindi katika Yesu, ambayo inaniambia Nguvu zisizoonekana na ambazo sio za kiMungu zinajaribu kunishinda.



Weka ukweli huu akilini: adui anakuja kuua, kuiba na kuharibu. Kila pepo lina malengo hayo. Jinsi wanavyoenda- njia na mikakati yao ipo tofauti. Roho ya kuogopa inashambulia imani, kwa mfano, wakati roho ya kukataa ina shambulia utambulisho. Shetani ana mikakati. Jeshi lake limejipanga hasa na anatuma roho maalum kushindana na waamini kudhohofisha ili kutoka kwenye kusudi lao la kifalme.



Maombi yangu ni kwamba utapata maarifa ya kutambua roho zinazo enda kinyume na maisha yako na maisha ya watu uwapendao na kuendelea kupigana kiroho. Utumwa wa kiroho unatokea katika njia tofauti, lakini habari njema ni kuwa Ushindi unaweza kuwa wetu. Kwa kutembea kwenye mamlaka tuliyo pewa na Mungu, tunaweza kupigana na kushinda vita kwa ufanisi

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Spiritual Warfare Battle Plan

Kwa haya mafundisho ya nguvu utaelewa kwa kina kuhusu jinsi ya kutengeneza njia ya kumpita adui na kuzuia mpango wake wa kuharibu maisha yako

Tunapenda kushukuru Charisma House kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://bit.ly/spiritualwarfarebattleplan

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha