Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Mpango wa kupigana Vita vya KirohoMfano

Spiritual Warfare Battle Plan

SIKU 2 YA 5

SIKU YA 2: Roho ya Yezebeli



Roho ya Yezebeli inatafuta kutongoza na mara nyingi hufanya kazi kupitia mafundisho na unabii. Roho hii huwatongoza watakatifu kufuata ibada za sanamu na uchafu. Roho inaweza kutumia kutawala na ujanja ili kufanya, lakini huo siyo mwisho wa mchezo. Mchezo wa mwisho wa Yezebeli ni kuua. Mshahara wa dhambi ni mauti, na Yezebeli anawaongoza watu katika dhambi.



Wachungaji-- au yeyote, kwa mfano--wanaoangukia katika dhambi ya uzinzi ni kati ya makombe ya Yezebeli. Kama unafanya kitu chochote kwa ajili ya Mungu, Yezebeli anataka kukata sauti yako. Kama Yezebeli hawezi kukata sauti yao, atajaribu kuipotosha sauti yako kwa kukushawishi kutia unajisi nafsi yako kwa kuvumilia kazi yake.



Yezebeli siyo kitu unaweza kukiangusha mara moja, lakini unaweza kuvunja agano nayo na kukataa kuvumilia.



Baba, ninatubu kwa kuvumilia Yezebeli na kuomba msamaha wako, katika jina la Yesu. Ninakuomba uponye moyo wangu kwa maumivu yanayoonekana na yasiyoonekana, vidonda, makosa, maumivu, kiburi, kukataliwa, uasi, au mlango wowote wazi unaoweza kuwa au ulioweza kumruhusu Yezebeli maishani mwangu.



Ninavunja uchawi wa Yezebeli, nguvu za kutawala, kudanganya, maneno ya laana, mashambulizi ya kutisha, mashitaka ya uongo, matamshi ya uongo wa kinabii, kutongoza kimapenzi, uchawi, vitisho, and kazi zingine za giza, katika jina la Yesu. Amen.


siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Spiritual Warfare Battle Plan

Kwa haya mafundisho ya nguvu utaelewa kwa kina kuhusu jinsi ya kutengeneza njia ya kumpita adui na kuzuia mpango wake wa kuharibu maisha yako

Tunapenda kushukuru Charisma House kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://bit.ly/spiritualwarfarebattleplan

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha