Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 03/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

SIKU 9 YA 31

Wamwaminio Yesu wameshikamana katika imani. Neno hili linatoa wito kwetu tushikamane mpaka mwisho. Mungu aliwahurumia wana wa Israeli akawatoa utumwani Misri kwenda Kanaani, lakini njiani walianguka katika dhambi, wakamkasirisha Mungu. Somo linasisitiza tusimame imara katika imani hata wakati wa majaribu. Leo ndiyo siku ya kutubu, kuamini na kutii, kesho ni kuchelewa. Waisraeli waliikosa nchi ya ahadi kwa kuasi na kutokuamini kwao. Nasi tusipoishi kwa imani, tutaikosa raha ya mbinguni.

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha ...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha