Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 03/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

SIKU 6 YA 31

Yesu alifanya suluhu kwa dhambi zetu (2:17,Ilimpasa kufafanishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake). Kwa hiyo Wakristo waitwawatakatifu(m.1), kwa kuwa walipokea msamaha wa dhambi kwa njia ya kumwamini. Ni watoto wa Mungu aliye mtakatifu. Waisraeli waliitwa taifa aunyumbaya Mungu, kwa kulishika agano la kale lililowafikia kupitia Musa (Hes 12:7,Mtumishi wangu, Musa, yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote). Yesu ni mkuu kuliko Musa, kama agano jipya lilivyo kuu kuliko agano la kale. Katika Agano Jipya neno linawaelekeza watoto wa Mungu kwa Yesu, ambaye kwa yeye tumefanywa washiriki wa mwito wa mbinguni.

Andiko

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 03/2024

Soma Biblia Kila Siku 03/ 2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha ...

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha