Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kufuata AmaniMfano

Pursuing Peace

SIKU 4 YA 7

Katika amani na sisi wenyewe

Mara nyingi vita vikuu dhidi ya amani ni vile ambavyo hutendeka ndani yetu. Kuna hadithi moja ambayo babu alimweleza mjukuu waka. "Ninahisi kana kwamba kuna mbwamwitu wawili wanaopigana rohoni mwangu. Mmoja ni mwenye kulipiza kisasi, mwenye hasira na vurugu. Mwengine ni mwenye upendo na huruma." Mjukuu naye akamwuliza, "Mbwamwitu yupi atashinda mapigano hayo?" Babu akajibu, " Yule ambaye ninamlisha."

Tunachagua chakula ambacho tunalisha roho zetu. Una mawazo yapi kujihusu? Lazima tupambane kila siku na mawazo yetu na tuwe waangalifu na jinsi ambavyo tunapambana na wasiwasi tuliokuwa nayo. Biblia inatuhimiza tutwike fadhaa zetu zote kwa Bwana na kumruhusu ahifadhi mioyo na nia zetu hata tusipoweza kuelewa ili tuwe na amani.

Methali ya Kiafrika:

Ngozi ya duma ni rembo ingawa moyo wake si mrembo. ~ Methali ya Kibaluba

Kuna makala challenging article Kuhusu 'Rhythms' ya Tearfund inayouliza iwapo utambulisho wetu unatokana na nguo tunazovaa.

Tendo:

Aghalabu tunapata utambulisho wetu kutoka kwa mali na mavazi yetu. Enda kwa duka la nguo ambalo unalipenda lakini si kununua kitu chochote. Tembea tu dukani ukifikiri mahitaji yako. Mpe Mungu sifa kwani anakuvika utakatifu wake. Omba akutane nawe hapo hapo. Enda nyumbani bila kununua kitu kwani ulikwenda ili kumtafuta kitu ambacho ni Mungu pekee anayeweza kukupa.

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Pursuing Peace

Tearfund inatafuta uongozi wa Mungu ili iwe sauti ya nguvu juu ya amani, mahusiano kurudishwa, na upatanifu kati ya jumuiya mbalimbali katika dunia. Somo hili la siku 7 lina matendo ya kila siku ili urudishe mahusiano ya...

More

Tungependa kushukuru Tearfund kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.tearfund.org/yv

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha