Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kufuata AmaniMfano

Pursuing Peace

SIKU 1 YA 7

Kuwa katika amani na Mungu

Wala si hivi tu, lakini tunafurahi katika Mungu kwa Bwana yetu Yesu Kristo, kwa yeye sasa tumepokea upatanisho. (Waroma 5:11)

Tunaweza kuanza kutafuta amani sisi wenyewe na peke yetu. Amani hupatikana katika mahali mengi. Ni vizuri kusudia kutafuta mahali pa kukutuliza iwe katika chemchemi ya maji yafaayo kama dawa, chumba cha michezo ya kuzoeza viungo vya mwili, au pahali popote panapokupumzisha.

Neno 'sanctuary' katika Kiingereza linatokana na neno la Kilatini 'sanctus' lenye maana ya takatifu. Tunapotafuta amani, tunapaswa kuwa na uangilifu tusishau kile kilicho kitakatifu.

Uhusiano wetu na Mungu umepatanishwa katika Yesu. Yesu alituleta katika uhusiano hai na Baba, unaoturuhusu kuitwa warafiki wa Mungu.

Kama kila urafiki wa maana, tunafaa kuwa wadhaifu na wenye kusema ukweli ile uhusiano uimarike. Nenda kwa Mungu na yale unayotaka kumpa, tafuta huruma ya upendo wake ikupatia amani. Muombe azidi kukuumba katika mfano wa Kristo.

Methali ya Kiafrika

Unionyeshe rafiki yako na nitakuonyesha tabia yako. ~ Methali ya kiafrika

Tendo:

Zungumuza na rafiki yako wa karibu na umwambie unayothamini katika urafiki wake. Baada ya ya mazungumuzo yale, waza namna unaweza imarisha uhusiano kama huo na Mungu, kwani amekuita rafiki yake.

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Pursuing Peace

Tearfund inatafuta uongozi wa Mungu ili iwe sauti ya nguvu juu ya amani, mahusiano kurudishwa, na upatanifu kati ya jumuiya mbalimbali katika dunia. Somo hili la siku 7 lina matendo ya kila siku ili urudishe mahusiano ya...

More

Tungependa kushukuru Tearfund kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea:http://www.tearfund.org/yv

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha