Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

SIKU 5 YA 30

Dhambi haiwezi kufanyika bila kupitia viungo vyetu, k.m. mkono au ulimi. Vinapotumika kutenda dhambi, Paulo anaviita “viungo vilivyo katika nchi”. Neno "vifisheni" si tafsiri nzuri. Ni afadhali kutafsiri "viache vife". Maana vile viungo havina ruhusa wala haki ya kumtawala aliyebatizwa, kwa sababu vimeshasulibishwa pamoja na Kristo, kama ilivyoandikwa katika Rom 6:6, Utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye [Yesu], ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena. Wakati vile viungo vinapotaka kutenda mabaya, tukumbuke kuwa nguvu ya dhambi imeshagongomewa msalabani, basi ibaki pale pale. Tumwache Yesu aifishe!

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha