Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

SIKU 1 YA 31

Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu (m.1). ”Injili” maana yake ni "habari njema". Kuja kwa Yesu Kristo kulikuwa mpango wa Mungu tangu awali. Kwa hiyo manabii wa A/K walitabiri juu ya jambo hili. Kwa mfano katika m.2-3 Marko ananukuu “kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya” (Isa 40:3) na Malaki (Mal 3:1). Fikiria jinsi inavyokuwa Rais anapotangaza kuzuru mahali fulani. Maandalio ya kumpokea ni mengi, barabara zinatengenezwa n.k. Kabla Yesu Kristo mwenyewe hajaja alitangulia mtu wa kumtengenezea njia. Yohana Mbatizaji alikuwa chombo teule cha Mungu cha kuwaandaa watu kiroho. Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao (m.4-5).

Andiko

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiun...

More

Tungependa Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha