Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Chuma Hunoa Chuma: Life-to-Life® Mentoring in the Old TestamentMfano

Iron Sharpens Iron: Life-to-Life® Mentoring in the Old Testament

SIKU 5 YA 5

Siku 5: Modekai na Esta



Mwanzoni tulimwangalia habari ya Naomi na Ruthu na tuliona jinsi mama mkwe alivyowajibika katika kumfundisha mkwewe. Hapa tunaona jinsi Mungu anavyoweza kukutumia kule mabadiriko katika maisha ya wanafamilia wengine kwa ajili ya umilele, hata binamu (au binti) wa jinsi tofauti.



Modekai aliishi Susa, Uajemi, katika kipindi cha uhamishoni cha watu wa Mungu. Alianza kumfundisha binamu yake yatima, Esta, ambaye alikuwa kama mkwe wake. Katika hatua hizo, tunaona jinsi alivyokuwa mtu sahihi kuambatana na Esta kwa wakati sahihi, na alikuwa mtu sahihi kusimama kati ya watu wa Mungu na maadui zake "kwa wakati kama huu"! 



Katika sura kumi za kitabu cha Esta, tunaona jinsi huyu binti mdogo asiyetarajiwa na kupanda na kuwa malkia. Kwa sababu ya ujana wake na kukosa uzoefu, na pia kuwa ni mateka wa Kiebrania, Esta alihitaji kupata mwongozo kutoka kwa mzee mwenye uzoefu.



Binamu yake Esta Modekai alimuongoza katika safari hiyo, na alimsikiliza, alipata kibali mbele ya wote waliomzunguka. Wakati mipango mibaya ilipoinuka ya kuwaangamiza Wayahudi katika nchi, Modekai alimuongoza Esta kila hatua kumwamini Mungu na kuomba kwa niaba ya watu wa Mungu.



Mungu aliingia kati! Siyo tu mafundisho ya Modekai yalibadilisha maisha ya Esta, bali pia yalibadilisha taifa. Mungu hakuwaokoa tuu watu wake, lakini pia alilinda hatimaye ujio wa Bwana Yesu Kristo!



Ukweli ni kwamba, hatujui Mungu amekusudia nini anapowaongoza na kututumia kutembea maisha kwa maisha na mtu mwingine. Ndiyo, Mungu anampenda kila mtu na anatamani kumwona akikua kila siku kuelekea utaua mkubwa. Wakati huo huo, kama tulivyoona kwenye uhusiano wa maisha kwa maisha tuliyoyaona, ni wazi kwamba Mungu siku zote anafanya kazi kwa njia za ajabu sana kutimiza kusudi lake katika ulimwengu huu- akiwatumia watu kama wewe na mimi katika hatua hiyo! 



Muhtasari huu wa mafundisho ya mahusiano ya maisha kwa maisha katika Agano la Kale yakusukume kuwekeza kwa wanao kuzunguka-- unapoishi, kufanya kazi, na kuomba!



_____



Tunapenda kumshukuru Dean Ridings, mwandishi wa The Pray! Prayer Journal, kwa ajili ya mpango huu.  Tafadhali pia tembelea, The Navigators.


siku 4

Kuhusu Mpango huu

Iron Sharpens Iron: Life-to-Life® Mentoring in the Old Testament

Unatamani "kufanya wanafunzi wanaofanya wanafunzi," kufuatana na Yesu katika Agizo Kuu (Mathayo 28:18-20)? Kama ndivyo, yawezekana umeona kwamba inaweza kuwa vigumu kupata watu wa mfano katika mchakato huu. Utafuata mfan...

More

Tunapenda kuwashukuru The Navigators kwa kutupa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: https://www.navigators.org/youversion

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha