Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Chuma Hunoa Chuma: Life-to-Life® Mentoring in the Old TestamentMfano

Iron Sharpens Iron: Life-to-Life® Mentoring in the Old Testament

SIKU 1 YA 5

Siku 1: Abraham na Lutu



Abraham anatupa moja ya mifano ya awali ya kumtengeza mtu katika Agano la Kale. Alitembea pamoja na mpwa wake Lutu, ambaye alimfuata kitoka katika mji wa kwao, Uru, kwenda kwenye nchi mpya iliyoahidiwa na Mungu.



Kutokea mwanzo, Abraham alikuwa ni mwalimu kwa mfano. Lutu alimwangalia Abraham alipokabiliana, aliposikia, na kuongea na Mungu. Alimwangalia Abraham alivyojenga madhabahu ya Bwana, aliyemtokea. Lutu aliangalia jinsi Abraham alivyokuwa akimtegemea Mungu, ambaye baadaye naye angeweka tumaini kwake.



Kadri Bwana alipowafanikisha wote, ukafika wakati ambapo ardhi ilikuwa haiwezi kutosha mifugo yao yote, wafugaji, na mahema yao, kwa hiyo ilibidi watengane. Kwa wema kabisa, Abraham akamwomba kwanza Lutu eneo ambalo angependa kukaa, na Abraham atakaa eneo lingine.



Tazama jinsi Abraham alivyokuwa anamwangalia mpwa wake. Alikuja kumwokoa alipokuwa anakabiliwa na shida, na kwa bidii alimuombea kwa niaba ya Lutu na familia yake wakati shida nyingine ilipoinuka.



Ni somo gani la matendo katika uhusiano wa maisha kwa maisha tunaweza kujifunza katika uhusiano huu? Kwanza, usidharau nguvu ya mfano binafsi! Kwa mfano wako, wewe ni mwalimu kwa wengi, hasa kwa wale mnaotembea pamoja kwa Karibu.



Pili, tunapaswa kuwaacha tunaowafundisha wachague njia yao wenyewe. Tutakuwa tu na muda mwingi nao, na lazima tuwaachilie katika uangalizi wa Mungu kwa muda mrefu. Wakati mwingine wanaweza kufanya maamuzi mabaya, au ya hatari (Mwanzo 19:8, 33,34). Wakati huohuo, hatuwaachilii kikamilifu waende. Tunabaki kuwa tayari kutumiwa na Mungu kusema ukweli kwenye maisha yao, kufanya yote tunayoweza kuwasaidia kuishi maisha marefu, maisha ya matunda katika Bwana.


siku 2

Kuhusu Mpango huu

Iron Sharpens Iron: Life-to-Life® Mentoring in the Old Testament

Unatamani "kufanya wanafunzi wanaofanya wanafunzi," kufuatana na Yesu katika Agizo Kuu (Mathayo 28:18-20)? Kama ndivyo, yawezekana umeona kwamba inaweza kuwa vigumu kupata watu wa mfano katika mchakato huu. Utafuata mfan...

More

Tunapenda kuwashukuru The Navigators kwa kutupa mpango huu. Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea: https://www.navigators.org/youversion

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha