Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 11/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11/2020

SIKU 6 YA 30

Wanawake na wanaume ni warithi pamoja wa neema ya uzima(m.7). Yaani kwa upande wa wokovu, wanawake na wanaume wako sawa kabisa. Lakini kwa upande wa wajibu na nafasi katika nyumba, wako tofauti. Mume hawezi kuwa na nguvu na kujisikia mwanamume kweli, mke wake asipomheshimu na kuwa na utii. Vilevile mke hawezi kuwa na nguvu na kujisikia mwanamke kweli, mume wake asipomheshimu na kumpenda. Wasipotimiza wajibu wao, maisha ya kiroho yanapata shida. Zingatia ilivyoelezwa katika m.3-4 kwamba kujipamba ... kuwa utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuumbele za Mungu. Na katika m.7 waume wanaambiwa kuwapa wake zao heshima na kukaa nao kama warithi pamoja wa neema ya uzima, kusudikuomba ... kusizuiliwe.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11/2020

Soma Biblia Kila Siku 11/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Kari...

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha