Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 08/2020Mfano

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

SIKU 2 YA 31

Swali la Petro lingeweza kuwa swali lako pia! Jambo hili la kumsamehe mtu aliyetukosea linatatiza sana wanadamu na hata Wakristo. Jibu la Yesu ni kwamba kusamehe kwetu kusiwe na mwisho, tena tusamehe kwa moyo (m.22:Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini. Na m.35: Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake). Na zaidi, Yesu anataka wewe uliyekosewa uchukue hatua ya kwanza ya kujaribu kupatanishwa na ndugu yako (m.15: Ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo). Yatawezekanaje haya? Mfano wa Yesu utakusaidia. Unahitaji sana kukumbuka na kutambua ukubwa wa deni la dhambi zako ambalo Mungu amekusamehe bure kwa neema yake!

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 08/2020

Soma Biblia Kila Siku 08/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Mathayo na Ezekieli na 2 Wakorintho. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mu...

More

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha