Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 11Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11

SIKU 3 YA 30

Yohana anaonyeshwa jinsi mambo yote yatakavyokuwa mapya. Tunajua kwamba Mungu hakai na wenye dhambi. Kwamba maskani yake sasa ni pamoja na wanadamu (m.3) inadhihirisha kwamba watu wamekuwa watakatifu. Imekuweje? Angalia katika m.5 ni nani anayefanya kila kitu kiwe kipya! Imeandikwa, Yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.Je, una shauku ya utakatifu huo walio nao wana wa Mungu? Basi ni wewe uliyekaribishwa kupokea ya chemchemi ya maji ya uzima, bure (m.6). Sasa hivi yapo maombolezo na maumivu, lakini tumeahidiwa ushindi na Yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu(m.7).

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11

Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha