Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 11Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11

SIKU 5 YA 30

Daudi alimpenda Bwana kwa moyo. Alikuwa mtiifu mbele ya Bwana. Kwa kila hatua ya maisha yake aliogopa kutokuyafuata mapenzi ya Mungu. Daudi akamwuliza Bwana ... Daudi akamwuliza Bwana tena ... Ee Bwana, Mungu wa Israeli, nakusihi, umwambie mtumwa wako. Naye Bwana akamjibu (m.2, 4 na 11). Kukosa utii mbele ya Bwana kulimfanya Sauli kukataliwa na Bwana. Samweli akasema, Je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, na kusikia kuliko mafuta ya beberu. Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi, na ukaidi ni kama ukafiri na vinyago; kwa kuwa umelikataa neno la Bwana, Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme(15:22-23). Vilevile kwetu Wakristo. Yesu hataki kuwa Mwokozi wetu tu. Anataka pia kuwa Bwana wetu. Tumfuate na kumtii katika yote! Yesu akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe? Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu(Lk 9:23-26).

siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11

Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha