Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 11Mfano

Soma Biblia Kila Siku 11

SIKU 30 YA 30

Mambo magumu sana yalipotukia kwa Daudi hayakumfanya amsahau au kumdharau Mungu, bali yalizidi kumfanya awe karibuna Mungu. Huenda alitunga Zab 143 kwa wakati huo. Kwa hiyo alipokuwa ameshinda matatizo, Daudi akatambua wazi kwamba ni kwa msaada wa Bwana na akampa utukufu.Ndipo Daudi akasema, La, ndugu zangu, msitende hivyo katika hizo nyara alizotupa Bwana, ambaye ndiye aliyetuhifadhi, akalitia mikononi mwetu lile jeshi lililokuja kinyume chetu(m.23). Basi Daudi alipofika Siklagi, aliwapelekea wazee wa Yuda, rafiki zake, sehemu ya nyara, akasema, Angalieni, zawadi yenu katika nyara za adui za Bwana(m.26). Bwana ana uwezo wa kuyageuza mabaya ili yawe baraka kwa mtu anayemtegemea. Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake(Rum 8:28). Pia tunaona Daudi ni mfano wa Kristo kwa kuwatendea wote haki na upendo!

siku 29

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 11

Soma Biblia Kila Siku 11 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Warumi na 1 Samweli.

Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha