Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kwa pamoja: Kutafuta maisha pamojaMfano

Collective: Finding Life Together

SIKU 6 YA 7

Hebu tuzungumze mahusiano ya jinsi tofauti na kusudi jinsi vinavyokwenda pamoja.  



Tumezungumza sana umuhimu wa mahusiano, lakini hebu tuzungumze kuhusu mahusiano ya jinsi tofauti. Kama mkristo, mahusiano ya jinsi tofauti yaweza kukukosesha amani- na ikawa ni somo lisilofaa. Yawezekana kwa sababu kuna ushauri wa aina nyingi kuhusiana na hilo ambao unaweza kutokuwa na manufaa.



Kwa wanaoanza, unaweza kuondoa baadhi ya msongo usiotakiwa unaosababishwa na mahusiano ya jinsi tofauti. Watu siku zote wanazungumza juu ya kumpata " mtu mwenyewe", na jambo hilo halipo. Hakuna mtu atayeweza kukufanya kamili. Ni Yesu tuu anayeweza kutosheleza hamu yako ya kujulikana, kuonekana, na kupendwa kwa jinsi ulivyo. Badala yake, unamtafuta mtu ambaye kwa bidii anamfuata Yesu ambaye anaweza kukusaidia kuwa mfuasi bora wa Kristo.



Hiyo pia haina maana mwaliko wa kahawa unaoenda hauwezi kuwa ni kutafuta majibu kwa sspwali lako la "je huyu anafaa kwa ndoa?" Unaweza kuwafahamu watu na kusikia habari zao. Zingatia katika kuanzisha urafiki na mtu yeyote unayetoka naye.



Hata hivyo, unaweza na unatakiwa kuweka mipaka ili na mahusiano yenye afya. Amua sasa jinsi utakavyo anzisha mahusiano. Weka mipaka utakapochora mstari kimwili, kiroho na kihisia.



Kuhusu kuweka mstari, hakikisha huukanyagi kuuzunguka. Lengo lako liwe - natakiwa nifanye nini ili kisichonifanya kuvuka mstari huo? Lengo lako liwe - mahusiano haya yanawezaje kuoeta heshima kwa Mungu? Ikiwa hilo ndiyo lengo lako, itakuwa rahisi sana kuweka mipaka sahihi kujilinda mwenyewe na maumivu yanayoweza kutokea baadaye.



Kunaweza pia kukawa na mvutano katika kuwa na mahusiano na kutimiza Kusudi lako, lakini haitakiwi kuwa hivyo. Usisubiri kufuata kusudi lako mpaka utakapokuwa kwenye mahusiano, kwa sababu hakuna mtu atakaye kukamilisha wewe.



Badala yake, muulize Mungu ni hatua ipi sahihi ya kuchukua- na ufanye hivyo. Subiri mahusiano kwa kusudi kwa kuishi kusudi lako.



Kuna msukumo mkubwa kwenda chuoni, kutafuta mahusiano, kuchumbia au kuchumbiwa, na kuoa au kuolewa. Hilo ni jambo jema kwa baadhi ya watu, lakini si hadithi ya watu wote. Na hiyo ni sawa! Futa matarajio kuhusu Kinachotakiwa Kutokea na ufurahie kipindi Mungu alichonacho kwako.



Ikiwa uko kwenye mahusiano ama la, Mungu ana mpango kwa ajili yako, kwa hiyo zingatia kufanya jambo sahihi na kumpenda zaidi Yesu. Kila kitu kitaenda sawa.



Fikiria: jinsi mahusiano yako ya baadaye( au sasa) yatakavyoonekana tofauti wakati lengo lako linapokuwa "Namna gani mahisiano haya yanaweza kuleta heshima kubwa kwa Mungu?" Badala ya "nitafanya nini ili nisivuke mstari?"



Omba: Mungu, nataka maisha yangu yakupendeze. Ikiwa ni pamoja na maisha yangu ya mahusiano! Nisaidie niwe na ujasiri na amani jinsi nilivyo na jinsi ulivyoniumba ili niishi kusudi langu kikamilifu- ikiwa sijaoa au nikiwa na mahusiano na mtu. Nisaidie kuwa mtu atayemuongoza yeyote nitakaye kuwa na mahusiano naye ili kuwa karibu zaidi na wewe. Katika jina la Yesu. Amen.


siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Collective: Finding Life Together

Unapofikia umri wa miaka 18, unaanza kuona kwamba unahitaji kupanga maisha yako. Itakuwaje usipofanya hivyo? Itakuwa kama ulipofikiria utakuwa sipo ulipo sasa? Hauko peke yako. Hebu tuangalie swali kuu la maisha yetu pam...

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha