Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kwa pamoja: Kutafuta maisha pamojaMfano

Collective: Finding Life Together

SIKU 4 YA 7

Je, watu wengine wananipenda? Je, najipenda mwenyewe?



Mitandao ya kijamii inaweza kutengeneza desturi ya kulinganisha. Ni kama ubao wa magoli wa kidigitali ambao haulali. Tunanaswa na mtego wa kulinganisha watu wangapi wamependa picha zetu dhidi ya mtu mwingine. Tunaona kundi la marafiki wakituma picha yao wakiwa kwenye burudani na kujiuliza—kwa nini sikualikwa? Kwa nini najisikia mpweke? 



Hiki ndicho tunapaswa kukitambua: Kitu ambachoo digitali inaweza kuwa danganyifu.Tunalinganisha maisha yetu yote na picha ya mtu mwingine. Taarifa tunayoiona inaweza kutufanya kufikiria kwamba maisha yao yamekamilika wakati sisi tunapambana bila kuonekana. Kiukweli, watu tunaowaone wako vizuri si ajabu nao wanajisikia kama sisi. Ni kwa sababu hatuoni upande wa pili.



Ndiyo maana inatupasa kuacha kujilinganisha na kushindana. Yesu alitufundisha sana kuhusu hili katika Mathayo 9:36. Katika hadithi ile, Yesu aliwaona makutano na akawahurumia.



Sasa hebu tuwe wakweli. Unapoona kundi la watu-unawahurumia au unajisikia kushindana?



Tukiona kushindana, hatuwezi kuwa na huruma, tutapoteza muunganiko wetu.



Kwa hiyo tuache mashindano hayo yasiyokuwa na mwisho badala yake chagua kushikiria utambulisho wetu katika Kristo. Hiyo inaonekanaje?



Utambulisho wako hautokani na unavyojisikia bali ujazo wa Roho Mtakatifu. Unapomfuata Yesu, roho yule yule aliyemfufua Yesu kutoka kwa wafu ndiye anakaa ndani yako. Kwa hiyo kwa siku unazojisikia hautoshi, unaweza kukumbuka kwamba kujisikia hubadirika, lakini Mungu wetu ni yeye yule jana, leo na hata milele. Na kwa sababu ya yale aliyoyafanya Yesu kwa ajili yetu, Mungu hazioni dhambi zako, anamuona mwanaye.



Umeumbwa kwa mfano wa Mungu. Unambeba Roho Mtakatifu ndani yako. Katika siku zako mbaya au siku zako bora zaidi, Mungu anakupenda, yuko kwa ajili yako, na alikuchagua. UsipoJisikia, soma neno la Mungu. Ukiri wako wa kila siku uwe na mizizi katika maandiko kukukumbusha Mungu anachosema wewe ni nani.



Unapojua wewe ni nani, unaweza kuacha kujilinganisha na kuanza kufurahia jinsi Mungu alivyomuumba kila mmoja wetu tofauti.



Fikiria: Unawezaje kuacha kujilinganisha na kuanza kufurahia wengine katika maisha yako? Unahitaji kuchukua hatua gani kuanza kuamini Mungu anachosema ulivyo.



Omba: Mungu, asante kwa ajili ya Yesu. Asante kwa neema yako na upendo wako. Nisaidie kukuamini na kujua unachosema juu yangu. Nisaidie kuacha kujilinganisha na wengine na kuanza kuwafurahia watu wanaonizunguka. Nipe huruma kwa ajili yangu na wengine wanaonizunguka. Katika jina la Yesu. Amen. 


siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Collective: Finding Life Together

Unapofikia umri wa miaka 18, unaanza kuona kwamba unahitaji kupanga maisha yako. Itakuwaje usipofanya hivyo? Itakuwa kama ulipofikiria utakuwa sipo ulipo sasa? Hauko peke yako. Hebu tuangalie swali kuu la maisha yetu pam...

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha