Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Kwa pamoja: Kutafuta maisha pamojaMfano

Collective: Finding Life Together

SIKU 5 YA 7

Unatambuaje kusudi lako la maisha?



Mara nyingi huwa tunawauliza watoto, "Unataka kuwa nani ukiwa mkubwa?"Ukifikiri, hili ni swali gumu sana kwa mtoto wa miaka 5. Ila unapofikia miaka 18, mara kuna shinikizo kubwa la kufanya maamuzi. Sasa swali kubwa ni hili-Ninapaswa kufanya nini na maisha yangu?



Bahati nzuri sana, Yesu anatupa mfumo maalum wa kufuata. Kama tulivyoongelea siku ya kwanza, kusudi kuu tulilo nalo ni kumpenda Mungu na kuwapenda watu. Linaonekana ni jambo rahisi sana, ila ni ngumu kuyaishi.



Kuwapenda watu inamaanisha kuwapenda hata pale wanapokosea, wanapokutenda vibaya, na pia wanapokukasirisha. Inamaanisha kila uamuzi unapitia kwenye lensikwa ajili ya kuchujwa ili kuona- Je uamuzi huu unaonyesha upendo kwa wengine wanaonizunguka?



Yesu alitupa uwazi zaidi kuhusiana na kusudi letu pale alipokuwa anawaacha wanafunzi wake. Katika maelekezo yake ya mwisho, Alitoa maelezo ya kusudi letu--twende kwa watu wote wa mataifa, tukawafanye wanafunzi wake na kuwafundisha kumtii Mungu. Pia aliahidi kuwa nasi katika kila nyanja.



Kusudi letu ni kuwaongoza watu kwa Yeshu kwa kuwapenda kama Yesu anavyowapenda. Jambo hili linaonekana ni rahisi, ila ni ngumu kulitenda. Haijalishi utaishia wapi, hilo ndilo kusudi lako kuu. Hata kama unafanya kazi kwenye ofisi, au kwenye kibanda cha kuuza kahawa, fanya lengo lako liwe kupenda watu wanaokuzunguka na kuwaeleza kuhusu Habari Njema za Yesu.



Tambua hili-si lazma ufanye jambo kubwa ndo uwe umefanya jambo la muhimu. Si lazma uwe Mkuu wa Kampuni au uende kwenye huduma au uwe bingwa kwenye jambo fulani ndio uwe umefanya mabadiliko. Mambo hayo yote ni mema, ila wote tunanafasi ya kufanya mambo makubwa kila siku kwa kuwapenda waliombele yetu.



Sasa ondoa shinikizo. Achana na matarajio yasiyo na lazima uliyojiwekea. Mungu yupo pamojanawe, anakulinda na kukuongoza kwenye njia Aliyokuandalia.



Bado hujaelewa jinsi ya kuridhia ukweli huu na maamuzi magumu na mengi yaliyo mbele yako?



Yafuatayo ni maswali matatu ya kukusaidia jinsi ya kuishi kusudi lako-ukiweka akilini kwamba unaweza kumpenda Mungu, kupenda wengine, na kuwafanya wafuasi Wake popote uendapo.



1. Katika uliyopitia zamani, lipi limekubadilisha zaidi? Haufafanuliwi kwa mambo uliyopitia, ila yatasaidia kukupata maelezo zaidi. Umewahi kupitia jambo linalokufanya kutaka kuwasaidia wengine katika jambo hilo? Hili linaweza kukusaidia kuamua ni jambo gani unalipendelea zaidi.



2. Je unajambo lolote linaloamsha hisia kali ndani yako? Nini kinaamsha hasira njema ndani yako? Kwa mfano, labda unajisikia hisia kali katika kuwalinda watoto walio katika mazingira hatarishi. Labda umekuwa ukivutiwa sana na kusaidia wagonjwa. Chochote kile, fikiri kama ukikifanya kama kazi kitakusaidia kufanya kile ambacho Mungu amekiweka ndani yako ukijali.



3. Ni kipawa kipi umebarikiwa nacho katika hali ya kawaida? Wote tunavipawa tofauti tulivyopewa na Mungu kwa ajili ya Utukufu wake. Ni jambo gani linakuja kwa urahisi kwako? Linaweza kukusaidia kuchagua cha kufanya.



Zingatia: Tumia muda kufikiri maswali hapo juu. Sali juu ya majibu yako, na pia jadili na watu wa karibu kwako. Angali kama muingiliano wa majibu yako yanaweza kukuonyesha kusudi lako.



Sali:Mungu Baba, Asante kwa kutupa vipawa na uwezo tofauti. Nisaidie niweze kukupenda Wewe na wanaonizunguka zaidi. Nisaidie niweze kufanya watu wafuasi wako. Nionyeshe ni eneo gani ninaweza Kukutumikia, na nionyeshe hatua yangu inayofuata ni ipi. Ninaomba haya kupitia kwa Mwanao Mpendwa Yesu Kristo. Amina.



siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Collective: Finding Life Together

Unapofikia umri wa miaka 18, unaanza kuona kwamba unahitaji kupanga maisha yako. Itakuwaje usipofanya hivyo? Itakuwa kama ulipofikiria utakuwa sipo ulipo sasa? Hauko peke yako. Hebu tuangalie swali kuu la maisha yetu pam...

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha