Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Usijisumbue kwa LoloteMfano

Anxious For Nothing

SIKU 5 YA 7

Huwa unajisikia kuhukumumiwa kwa kuwa Mkristo ambaye "hasumbuki kwa lolote"? Je kuogopa kunakuketea uoga zaidi kwa sababu unajisikia kama hukutakiwa kuogopa? Lori alikuwa katika hali hiyohiyo mpaka alipogundua jambo moja ambalo lilibadilisha kila kitu. 



Ndoa yangu ilikuwa imevurugwa. Nilikuwa nabeba jukumu lote la kulea watoto watatu, wawili wao vijana ( Bwana nisaidie!) yote kwangu. Kufanya kazi, kupika, kusafisha, kuosha magari, kutengeneza, kugharamia, kutegemeza, kuwapenda, kila kitu kwangu. Hofu yangu ilikuwa kubwa, na sikujua nifanye nini.



Nilikuwa najaribu kila nilichoweza: ushauri, kutafakari, madawa, muziki, mazoezi, kukariri maandiko, chochote unachoweza kukifikiria. Hakuna kilichoweza kuondoa hofu. Usinielewe vibaya, ni wazi ilikuwa inasaidia kufanya vitu hivi. Nilijifunza kutumia zana nilizozihitaji kuweza kurudi katika Yesu. Lakini bado nilikuwa nahangaika. Nikiangalia nyuma, jambo moja niligundua kuwa sikuwa najaribu ni "kutokujaribu.”



Kama ukiyachunguza maandiko, utapata lundo la mistari kuhusiana na hofu. Ninajua kwa sababu nilikuwa natafuta njia ya ajabu kubisaidia kushinda hofu kabisa. Katika utafiti wangu, nilipata kitu bila kutarajia. Lazima uwe makini ili uweze kukiona, lakini mistari hii ni maelekezo kutoka kwa Baba yetu kutokujisumbua kwa lolote. Ndiyo, kwa uhakika--chochote.



Katika Mathayo 11:28 SUV, Yesu Kuja, Jesus says, ““Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.” Anafanya kazi hapa, siyo sisi. Tunatakiwa kuja kwake tuu.



Katika Yohana 14:27 SUV, anasema, “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga." Unaelewa somo? Anatupa amani. Anatupa pumziko. Hakuna tunachofanya sisi.



Tena katika Mathayo 6:25-34 SUV, kifungu hiki maarufu kinatuambia tusiogope, kwa kuwa Mungu " huvisha majani ya kondeni", si zaidi sana sisi? Tumeambiwa " kuutafuta kwanza ufalme wake ... na hayo yote tutapewa". Ni sahihi-- umeipata hiyo? Tutapewa!



Mungu ni mpaji. Ana majibu, na anatujali. Vitu hatuwezi kuvifanya, na hivyo ndivyo alivyoviweka. Sisi kumtafuta.



Vitu vyote ambavyo niliviogopa, vilitimia, kimoja baada ya kingine. Haikuwa hivyo mpaka nilipoamua, kupumzika, kuja kwa Yesu, nilipotulia, na kuacha yote yapite, kumwambia Mungu ninamtegemea kikamilifu--na nilijifunza kumwachia--mwishowe nikapata amani. Mwishowe, maombi yangu yakapungua kuhusu hali yangu na yakazidi katika tumaini langu kwake. 



Ukifanya hivyohivyo, ninakutia moyo kutulia kwake. Unaweza kumtumaini. Huna naomba hivi naposikia kuzidiwa na hofu tena:



Bwana wangu,



Nakuja kwako leo na nakuomba unisaidie. Wewe ni yote kwangu. Bwana, nahitaji pumziko. Ninakupa uoga wangu. Uchukue Bwana. Napokea amani yako, upendo, na ufahamu. Nisaidie kukugeukia na nisijiangalie mwenyewe. Nisaidie kuacha kufanya na nianze kutumaini. Nisaidie kusubiri majibu yako, kwa sababu najua ni mazuri. Nipe hekima, tumaini, na amani. Asante Bwana, kwa uvumilivu wako na neema. Ninakupenda, na najua unanipenda sana kuliko navyoweza kufikiria.



Amen.



-Lori


siku 4siku 6

Kuhusu Mpango huu

Anxious For Nothing

Ingekuwaje kama kungekuwa na njia bora ya kupigana na hofu isiyoisha inayokufanya kukosa usingizi? Pumziko halisi lipo--yawekana karibu zaidi ya unavyofikiria. Badilisha hofu na amani kupitia siku hizi 7 za mpango wa Bib...

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha