Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Usijisumbue kwa LoloteMfano

Anxious For Nothing

SIKU 4 YA 7

Yesu hukutana nasi katikati ya hofu, hata kama hatumhisi mwanzoni. Chelsea mwanzoni alipata uzoefu wa hofu mara baada ya kuhitimu chuo. Hadithi yake ya jinsi Mungu alivyomtoa kwenye giza mpaka kwenye amani yake. 



Kujisikia hofu, mashaka, na msongo ilikuwa halisi. Nilishindwa hata kula kwa sababu ya kichefuchefu. Nililala zaidi ya masaa 12 usiku, bado asubuhi ilikuwa ni vita mimi kuamka kutoka kitandani. Nilisongwa sana na mawazo yangu mwenyewe kiasi kwamba mara nyingi nilishindwa hata kusema. Nilitafuta msaada kwenye familia yangu, kwa daktari, kwa mshauri, kwa wachungaji, na marafiki, siku zangu za giza zilionekana kutokwisha.



Wote tunapitia siku za giza. Na siku hizo zinaweza kudumu juma zima. Au miezi. Au miaka. Lakini kama unajua hadithi ya Ijumaa Kuu, siku Yesu alipotoa maisha yake kwa ajili yako, unajua kuna habari njema, rafiki. Ijumaa ni giza, lakini Jumapili inakuja!



Tuna tumaini katika giza, na tumaini letu lina jina. Jina lake ni Yesu. 



Katika siku yangu ya giza nene, Ijumaa ya mwezi Julai, hatimaye nilimkaribia kama ambavyo amekuwa akinikaribia. Niliomba: 



Yesu, nisaidie kukataa uongo wa adui.

Yesu, nisaidie kushinda hofu ya moyo wangu.

Yesu, nisaidie kuamini kwamba unatawala.

Yesu, nisaidie kuamini kwamba Roho aliyekufufua kutoka kwa wafu anaishi ndani yangu.



Na siku mbili baadaye, Jumapili, niliamka pasipo na msongo na pasipo kusikia hofu. Kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu, niliweza kupata amani yake. Na nilipata muujiza wa uponyaji ambao unaweza kuelezewa kwa wema wa Mungu.



Wakati wa siku zangu za giza, Yesu alinipa tumaini. Hata nilipokuwa simhisi, alikuwepo. Kila siku nilipojisikia kuwa mbali naye, alikuwa ananivuta karibu naye.



Sijui kama utapata muujiza wa haraka wa uponyaji kutokana na maumivu yako kama mimi. Lakini najua kwa uhakika Mungu yupo nawe kwenye maumivu.



Yesu anajuma mateso mwanadamu. Na anajali. Alijali sana kiasi cha kuacha mbingu na kufa kwa ajili yetu kuondoa giza letu mara moja. 



Biblia inasema: … Maisha yake yalileta mwanga kwa kila mtu. Nuru hunga'aa gizani, giza haliwezi kuushinda mwanga. Yohana 1:4-5 SUV



Jumapili yaja. 



-Chelsea  


siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Anxious For Nothing

Ingekuwaje kama kungekuwa na njia bora ya kupigana na hofu isiyoisha inayokufanya kukosa usingizi? Pumziko halisi lipo--yawekana karibu zaidi ya unavyofikiria. Badilisha hofu na amani kupitia siku hizi 7 za mpango wa Bib...

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha