Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Usijisumbue kwa LoloteMfano

Anxious For Nothing

SIKU 2 YA 7

Itakuwaje kama hofu inaweza kukuleta karibu na Yesu? Jordan alitumia mwaka mzima kufukuza hofu mpaka alipogundua kitu cha ndani zaidi--uhusiano wa karibu na Yesu. Yawezekana unaweza kufananisha na hadithi hii: 



“Nadhani nitakufa.”



Hicho ndicho nilichofikiria nilipokosa usingizi mara nyingi mwaka uliopita. Nilijaribu kupata usingizi, ghafla naamshwa na uoga pasipokuwa na sababu maalum. Kifua kilikuwa kimejaa. Nilijisikia kama nakabwa, na sikuweza kupumua wakati mwingine. Mzunguko huo ungejirudua, na hatimaye niliamua kulala kwenye kochi ili niache kumwamsha mke wangu. 



Siku moja, nilenda kwa daktari na kumwelezea dalili zangu-- maumivu ya kifua, shida ya kupata usingizi, na mashambulizi ya uoga. Baada ya vipimo kadha kwa muda niliomuona, alinikuta kuwa nina hofu. Naweza kuwa muwazi? Ilinifanya nijisikie kama mtu aliyeshindwa kama Mkristo. Nisingekuwa naombea kinyume na hili moja kwa moja? Sitakiwi kushughulika na hili, Nitalifikiria mwenyewe, nilitakiwa kuwa na amani siyo hofu--ndicho Yesu alichosema kufanya!



Baada ya kufuata maelekezo ya daktari na kuanza kunywa dawa, niliendelea kuomba hofu iondoke. Sikutaka kushughulika nayo tena.



Katika 2 Wakorintho 12, katika tafsiri ya SUV, Paulo anaeleza " mwiba katika mwili." Japo hatujui kwa uhakika "mwiba" wa Paulo kilikuwa kitu gani, hofu inaweza kwa uhakika kuwa kwa watu wengi, na mimi nikiwemo. Paulo anasema alimsihi Bwana mara tatu auondoe, lakini badala yake, Yesu alimwambia, “Neema yangu yakutosha, kwa maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu.” (emphasis added)



Neema ya Yesu yatosha, haijalishi ni katika mazingira gani. Nilipoanza kuomba kwa ajili ya uponyaji, nilianza kuwa karibu na Yesu. Kama Paulo, Mungu hajaondoa "mwiba" wangu. Hata hivyo, nimejikuta napenda zaidi kusoma neno lake, nimeomba kuliko nilivyowahi kuomba huko nyuma.



Nilidhani nilichohitaji ni uponyaji wa hofu yangu. Kusema ukweli, nilimuhitaji zaidi Yesu. Sasa, sisemi kama ningekuwa karibu na Yesu kwamba nisingekuwa na hofu. Sitaacha kuendelea kuomba ili hofu iondoke. Naendelea kuomba ili nifunguliwe kutokana na mwiba huu kama Paulo alivofanya. 



Lakini kuna kitu bora zaidi kinatokea kwangu zaidi ya kupata uponyaji wa papo kwa papo wa hofu. Ninajenga ufahamu wa ndani wa Mungu na uhusiano wa karibu naye.



Badala ya kuomba kwa ajili ya amani tuu, nimejikuta nakuwa karibu zaidi na Mfalme wa Amani. Nilipoanza kuhofia maisha yangu ya baadaye, nilijikumbusha kwamba yeye ni Alfa na Omega-- mwanzo na mwisho, wa kwanza na wa mwisho.



Niliomba hofu yangu initoke, lakini nilipata kilicho bora: wingi wa uwepo wa upendo wa Yesu katika maisha yangu-- hata katikati ya hofu.



-Jordan


siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

Anxious For Nothing

Ingekuwaje kama kungekuwa na njia bora ya kupigana na hofu isiyoisha inayokufanya kukosa usingizi? Pumziko halisi lipo--yawekana karibu zaidi ya unavyofikiria. Badilisha hofu na amani kupitia siku hizi 7 za mpango wa Bib...

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha