Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Yesu Mfalme: Ibada ya Pasaka na Timothy KellerMfano

JESUS THE KING: An Easter Devotional By Timothy Keller

SIKU 2 YA 9

“Uponyaji wa Kina Zaidi”



Yesu anajua kitu ambacho bado mtu huyo hajatambua— ya kuwa ana shida kubwa zaidi ya hali yake ya kimwili. Yesu anamwambia, "Naelewa shida zako. Nimeona mateso yako. Nitayafikia. Lakini tafadhali tambua ya kwamba tatizo kuu katika maisha ya mwanadamu sio mateso yake; ni dhambi zake"



Iwapo majibu ya Yesu yanakukera, tafadhali fikiria hivi: ikiwa mtu anakuambia, "Tatizo kuu maishani mwako sio kilichokutendekea , si kile watu wamekufanyia; tatizo lako kuu ni jinsi ulivyoitikia"—kinaya ni kwamba jibu hilo ni la kuwezesha. Kwa nini? Kwa sababu huwezi kufanya mengi kuhusu yaliyokutendekea au kuhusu yale wengine wanafanya—lakini unawezakudhibiti matendo yako mwenyewe. Biblia inapozungumzia dhambi, haimaanishi tu yale mambo mabaya tunayoyafanya. Sio tu uongo au tamaa—ni kupuuza Mungu katika dunia aliyoumba; ni kuasi Mungu kwa kuishi maisha bila ya kumrejelea. Ni kusema, "Nitaamua kikamilifu jinsi nitakavyoishi maisha yangu." Na Yesu anasema kuwa hilo ndilo tatizo letu kuu.



Yesu anamkabili mtu yele aliyepooza na tatizo lake kuu kwa kumwelekeza atazame kwa kina zaidi. Yesu anasema,"Kwa kuja kwangu na kuomba mwili wako uponywe pekee, hautazami kwa kina inayofaa . Umepuuza kina cha matarajio yako, matarajio ya moyo wako." Kila mtu aliyepooza kawaida anataka kwa hali yake yote apone na aweze kutembea. Lakini hakika huyu angekuwa ameweka matumaini yake yote katika uwezekano wa kutembea tena. Yamkini moyoni mwake anasema, "Kama tu ningeweza kutembea tena, basi maisha yangekuwa laini. Sitawahi kuwa mwenye huzuni kamwe, sitawahilalamika. Ikiwa tu ningetembea, basi kila kitu kingekuwa shwari." Na Yesu anasema, "Mwanangu, umekosea." Pengine inaonekana katili, lakini ni kweli kabisa. Yesu anasema, "Ninapoponya mwili wako, kama nitatenda hayo tu, utajihisi kwamba hutahuzunika tena. Lakini ngoja miezi miwili, miezi minne—msisimko huo hautadumu. Mizizi ya kutoridhika kwa moyo wa mwanadamu ni ya kina."



Ni kwa nini msamaha ulikuwa kitu alichohitaji zaidi mtu aliyepooza? Ni kwa nini msamaha ni hitaji letu la kina zaidi? Ni "mahitaji" yapi mengineyo tunaona ni ya kina zaidi kuliko hitaji la msamaha?



Nukuu kutoka JESUS THE KING na Timothy Keller

Imechapishwa tena kwa mpangilio na Riverhead Books, mshiriki wa kundi la Penguin (USA) LLC, Kampuni ya Penguin Random House Haki Miliki © 2011 na Timothy Keller



na kutoka JESUS THE KING STUDY GUIDE nao Timothy Keller and Spence Shelton, Haki Miliki (c) 2015 na Zondervan, tawi la uchapishaji la HarperCollins Christian.



Andiko

siku 1siku 3

Kuhusu Mpango huu

JESUS THE KING: An Easter Devotional By Timothy Keller

Mwandishi maarufu wa New York Times na mchungaji mashuhuri Timothy Keller anatuletea mfululizo wa vipindi katika maisha ya Yesu kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Marko. Tunapomakinika katika hadithi hizi, anatuletea u...

More

Vifungu kutoka kwa Riverhead Books, mwanachama wa Penguin Random House, Mwongozo kutoka Harper Collins Christian Publishers. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.penguin.com/book/jesus-the-king-by-timothy-keller/9781594486661 ama http://www.zondervan.com/jesus-the-king-study-guide

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha