Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Yesu Mfalme: Ibada ya Pasaka na Timothy KellerMfano

JESUS THE KING: An Easter Devotional By Timothy Keller

SIKU 7 YA 9

“Komunyo na Ushirika”



Kumbuka alichosema Yesu alipochukua kikombe:



Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa; wakakinywea wote. Akawaambia “Hii ndiyo damu yagu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi. Amin, nawaambia ninyi, sitakunywa tena kabisa uzao wa mzabibu, hata siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu.”

(Marko 14:23–25)



Maana ya maneno ya Yesu ni kwamba matokeo ya dhabihu yake ambapo alijitolea kuwa mbadala ni agano jipya kati yetu na Mungu. Na msingi wa uhusiano huu ni damu yake Yesu mwenyewe: “damu yangu ya agano.” Anapotangaza kwamba hatakula wala kunywa hadi atakapokutana nasi katika ufalme wa Mungu, Yesu anaahidi kuwa yeye ni mwaaminifu bila masharti kwetu: “Nitawaleta mikononi mwa Baba. Nitawaleta karamuni mwa Mfalme.” Mara nyingi Yesu analinganisha ufalme wa Mungu na kuketi katika karamu mkuu. Katika Mathayo 8, Yesu anasema, “Nami nawaambieni, ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi . . . katika ufalme wa mbinguni.” Yesu anaahidi kwamba tutakuwa katika karamu ya ufalme pamoja naye.



Akitumia ishara hizi sahili ya kuinua mkate na divai, na maneno sahili “Huu ni mwili wangu . . . hii ni damu yangu,” Yesu anasema kwamba wokovu wote wa awali, dhabihu zote za awali, wanakondoo wote wa Pasaka, ulikuwa mwelekezo kwake. Kama vile Pasaka ya kwanza iliadhimishwa usiku kabla Mungu awakomboe Wanaisraeli kutoka utumwani kupitia damu ya wanakondoo, huu mlo wa Pasaka utaliwa usiku kabla Mungu akomboe ulimwengu kutoka kwa dhambi na kifo kupitia damu ya Yesu.



Ni vitu vipi vinavyohitajika kutendeka moyoni na akilini mwako ili uweze kupokea kwa dhati anachokutolea Yesu?



Nukuu kutokwa kwa JESUS THE KING cha Timothy Keller

kuchapishwa kwa mpangilio na Riverhead Books, mshiriki wa kikundi cha Penguin (USA) Kampuni ya Penguin Random House. Haki Miliki © 2011 na Timothy Keller



Na kutoka kwa JESUS THE KING STUDY GUIDE nao Timothy Keller na Spence Shelton, Haki Miliki (c) 2015 na Zondervan, tawi la wachapishaji wa HarperCollins Christian.

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

JESUS THE KING: An Easter Devotional By Timothy Keller

Mwandishi maarufu wa New York Times na mchungaji mashuhuri Timothy Keller anatuletea mfululizo wa vipindi katika maisha ya Yesu kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Marko. Tunapomakinika katika hadithi hizi, anatuletea u...

More

Vifungu kutoka kwa Riverhead Books, mwanachama wa Penguin Random House, Mwongozo kutoka Harper Collins Christian Publishers. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.penguin.com/book/jesus-the-king-by-timothy-keller/9781594486661 ama http://www.zondervan.com/jesus-the-king-study-guide

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha