Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Yesu Mfalme: Ibada ya Pasaka na Timothy KellerMfano

JESUS THE KING: An Easter Devotional By Timothy Keller

SIKU 6 YA 9

“Kufanya Yasiyowezekena Yawezekane”



Katika tukio hili, Yesu anasema kwamba pana kitu ambacho ni kasoro kubwa ndani yetu sisi sote—lakini pesa ina nguvu ya kipekee ya kutupofusha. Kwa kweli, ina nguvu mno sana wa kutudanganya kuhusu hali yetu ya kiroho hadi tunahitaji Mungu aingilie kati kwa miujiza na neema ili tuitambue. Haiwezekani bila Mungu, bila miujiza. Bila neema.



Chukua namna ambavyo Yesu alishauri kijana huyu. Naam, mvulana huyu alihitaji ushauri, ingawa nje alionekana kana kwamba alikuwa shwari. Alikuwa tajiri, ni kijana, na pengine mtanashati—ni ngumu kuwa tajiri na kijana ilhali wewe si mtanashati. Lakini hakuwa shwari. Iwapo angekuwa, hangeend kwa Yesu na kuuliza, “Nifanye nini kuurithi uzima wa milele?”



Myahudi yeyote aliyekuwa mcha Mungu angejua jibu la swali hili. Walimu daima walikuwa wakiuliza swali hili katika maandiko yao na mafunzo yao. Na jibu lilikuwa lile lile; hapakuwa na nadharia tofauti kulihusu. Jiby lilikuwa “Shika amri za Mungu na ujitenge na dhambi zote.” Kijana angejua jibu hili. Mbona basi alimwuliza Yesu?



Tamko la busara la Yesu kwamba “Umepungukiwa na neno moja” linaturuhusu kubaini kiini cha mapambano ya kijana huyu. Mwanaume alikuwa anasema, “Unajua, nimefanya kila kitu kwa njia sahihi: nimefanikiwa kiuchumi, kijamii, kimaadili, kidini. Nimesikia kwamba wewe ni mwalimu mzuri, na ningependa kujua iwapo kuna kitu ambacho nimekosa, ambacho nimepuuza. Ninahisi kwamba kuna kasoro mahali.”



Bila shaka alikuwa amekosa kitu. Kwa sababu yeyote anayetegemea matendo yake kupata uzima wa milele atapata kwamba, ingawa ametimiza mengi, pana utupu, wasiwasi, shaka. Lazima ipo kasoro fulani. Je, mtu atajuaje kwamba amefika kiwango?



Je, unaweza kutafuta fanaka katika kazi yako bila kunaswa katika mtego ambao mali unatega? Ni njia zipi ambazo injili imebadili—au unaweza kubadili—mtazamo wako kuhusu pesa?



Nukuu kutokwa kwa JESUS THE KING cha Timothy Keller

kuchapishwa kwa mpangilio na Riverhead Books, mshiriki wa kikundi cha Penguin (USA) Kampuni ya Penguin Random House. Haki Miliki © 2011 na Timothy Keller



Na kutoka kwa JESUS THE KING STUDY GUIDE nao Timothy Keller na Spence Shelton, Haki Miliki (c) 2015 na Zondervan, tawi la wachapishaji wa HarperCollins Christian.

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

JESUS THE KING: An Easter Devotional By Timothy Keller

Mwandishi maarufu wa New York Times na mchungaji mashuhuri Timothy Keller anatuletea mfululizo wa vipindi katika maisha ya Yesu kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Marko. Tunapomakinika katika hadithi hizi, anatuletea u...

More

Vifungu kutoka kwa Riverhead Books, mwanachama wa Penguin Random House, Mwongozo kutoka Harper Collins Christian Publishers. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://www.penguin.com/book/jesus-the-king-by-timothy-keller/9781594486661 ama http://www.zondervan.com/jesus-the-king-study-guide

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha