Zaburi 65:11-13
Zaburi 65:11-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Wautunukia mwaka wote mema yako, kila ulipopitia pamejaa fanaka. Mbuga za majani zimejaa mifugo, milima nayo imejaa furaha. Malisho yamejaa kondoo, mabonde yamefunikwa kwa ngano. Kila kitu kinashangilia kwa furaha.
Zaburi 65:11-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Umeuvika mwaka taji la wema wako; Mapito yako yadondoza unono. Huyadondokea malisho ya nyikani, Na vilima vimejawa na furaha. Na malisho yamejawa na kondoo, Na mabonde yamepambwa nafaka, Yanashangilia, na kuimba pamoja kwa shangwe.
Zaburi 65:11-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Umeuvika mwaka taji ya wema wako; Mapito yako yadondoza unono. Huyadondokea malisho ya nyikani, Na vilima vyajifunga furaha. Na malisho yamevikwa kondoo, Na mabonde yamepambwa nafaka, Yanashangilia, naam, yanaimba.
Zaburi 65:11-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Umeuvika mwaka taji ya baraka, magari yako yanafurika kwa wingi. Mbuga za majani za jangwani umezineemesha; vilima vimevikwa furaha. Penye nyanda za malisho pamejaa makundi ya wanyama, na mabonde yamepambwa kwa mavuno; vyote vinashangilia kwa furaha na kuimba.