Zaburi 41:1-3
Zaburi 41:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Heri mtu anayewajali maskini; Mwenyezi-Mungu atamwokoa wakati wa shida. Mwenyezi-Mungu atamlinda na kumweka hai, naye atafanikiwa katika nchi; Mungu hatamwacha makuchani mwa maadui zake. Mwenyezi-Mungu atamsaidia awapo mgonjwa, atamponya maradhi yake yote.
Zaburi 41:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Heri amkumbukaye mnyonge; BWANA atamwokoa siku ya taabu. BWANA atamlinda na kumhifadhi hai, Naye atafanikiwa katika nchi; Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake. BWANA atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani. Katika ugonjwa wake unamponya maradhi yake yote.
Zaburi 41:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Heri amkumbukaye mnyonge; BWANA atamwokoa siku ya taabu. BWANA atamlinda na kumhifadhi hai, Naye atafanikiwa katika nchi; Wala usimtie katika hali wamtakiayo adui zake. BWANA atamtegemeza alipo mgonjwa kitandani. Katika ugonjwa wake umemtandikia.
Zaburi 41:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Heri mtu yule anayemjali mnyonge, BWANA atamwokoa wakati wa shida. BWANA atamlinda na kuyahifadhi maisha yake, atambariki katika nchi na hatamwacha katika tamaa ya adui zake. BWANA atamtegemeza awapo mgonjwa kitandani, atamwinua kutoka kitandani mwake.