Zaburi 128:1-6
Zaburi 128:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Heri wote wamchao Mwenyezi-Mungu, wanaoishi kufuatana na amri zake. Utapata matunda ya jasho lako, utafurahi na kupata fanaka. Mkeo atakuwa kama mzabibu wa matunda mengi nyumbani mwako; watoto wako kama chipukizi za mzeituni kuzunguka meza yako. Naam, ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu akubariki kutoka Siyoni! Uione fanaka ya Yerusalemu, siku zote za maisha yako. Uishi na hata uwaone wajukuu zako! Amani iwe na Israeli!
Zaburi 128:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Heri kila mtu amchaye BWANA, Aendaye katika njia yake. Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema. Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Katika nyumba yako. Wanao watakuwa kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako. Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye BWANA. BWANA akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako; Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.
Zaburi 128:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Heri kila mtu amchaye BWANA, Aendaye katika njia yake. Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema. Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Vyumbani mwa nyumba yako. Wanao kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako. Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye BWANA. BWANA akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako; Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.
Zaburi 128:1-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Heri ni wale wote wamchao BWANA, waendao katika njia zake. Utakula matunda ya kazi yako; baraka na mafanikio vitakuwa vyako. Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao ndani ya nyumba yako; wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni kuizunguka meza yako. Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa mtu amchaye BWANA. BWANA na akubariki kutoka Sayuni siku zote za maisha yako, na uone mafanikio ya Yerusalemu, nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako.