Wafilipi 3:1-2
Wafilipi 3:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika kuungana na Bwana. Sichoki kurudia yale niliyokwisha andika pale awali, maana yatawaongezeeni usalama. Jihadharini na hao watendao maovu, hao mbwa, watu wanaosisitiza kujikata mwilini.
Wafilipi 3:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana. Kuwaandikieni mambo yale yale hakuniudhi mimi, bali kutawafaa ninyi. Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao.
Wafilipi 3:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana. Kuwaandikieni mambo yale yale hakuniudhi mimi, bali kutawafaa ninyi. Jihadharini na mbwa, jihadharini na watendao mabaya, jihadharini na wajikatao.
Wafilipi 3:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana! Mimi kuwaandikia mambo yale yale hakuniudhi, kwa maana ni kinga kwa ajili yenu. Jihadharini na mbwa, wale watenda maovu, jihadharini na wale wajikatao miili yao, wasemao ili kuokoka ni lazima kutahiriwa.