Yobu 37:8-11
Yobu 37:8-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Wanyama wa porini hurudi mafichoni mwao, na hubaki katika mapango yao. Dhoruba huvuma kutoka chumba chake, na baridi kali kutoka ghalani mwake. Kwa pumzi ya Mungu barafu hutokea, uso wa maji huganda kwa haraka. Mungu hulijaza wingu manyunyu mazito; mawingu husambaza umeme wake.
Yobu 37:8-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hapo wanyama huingia mafichoni, Na kukaa katika mapango yao. Dhoruba hutoka katika vyumba vyake; Na baridi ghalani mwake. Kwa pumzi ya Mungu barafu hutokea; Na uso wa maji huganda punde. Naam, huyatwika mawingu mazito mzigo wa maji; Hulitandika wingu la umeme wake
Yobu 37:8-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hapo wanyama huingia mafichoni, Na kukaa katika mapango yao. Dhoruba hutoka katika vyumba vyake; Na baridi ghalani mwake. Barafu huletwa kwa pumzi za Mungu; Na upana wa maji huganda. Naam, huyatweka mawingu mazito mzigo wa maji; Hulitandika wingu la umeme wake
Yobu 37:8-11 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wanyama hujificha; hubakia kwenye mapango yao. Dhoruba hutoka katika chumba chake, baridi hutoka katika upepo uendao kasi. Pumzi ya Mungu hutoa barafu, eneo kubwa la maji huganda. Huyasheheneza mawingu kwa maji, naye husambaza umeme wake wa radi kupitia hayo.