Yeremia 23:36-37
Yeremia 23:36-37 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini jambo la ‘Mzigo wa Mwenyezi-Mungu,’ msilitaje tena. Kile anachosema binadamu ni mzigo kwake mwenyewe. Watu wanayapotosha maneno ya Mungu aliye hai, Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wao. Basi mtamwuliza nabii hivi: ‘Mwenyezi-Mungu amekujibu nini?’ au, ‘Mwenyezi-Mungu amesema nini?’
Yeremia 23:36-37 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na mzigo wa BWANA hamtautaja tena; maana neno la kila mtu ndilo litakalokuwa mzigo wake; maana ninyi mmeyapotosha maneno ya Mungu aliye hai, ya BWANA wa majeshi, Mungu wetu. Nawe utamwambia nabii hivi, BWANA amekujibu nini? Na, BWANA amesemaje?
Yeremia 23:36-37 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na mzigo wa BWANA hamtautaja tena; maana neno la kila mtu ndilo litakalokuwa mzigo wake; maana ninyi mmeyapotosha maneno ya Mungu aliye hai, ya BWANA wa majeshi, Mungu wetu. Nawe utamwambia nabii hivi, BWANA amekujibu nini? Na, BWANA amesemaje?
Yeremia 23:36-37 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini kamwe msiseme tena, ‘Nina mzigo wa BWANA,’ kwa sababu kila neno la mtu binafsi linakuwa mzigo wake mwenyewe, na hivyo kupotosha maneno ya Mungu aliye hai, BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mungu wetu. Hivi ndivyo utakavyoendelea kumuuliza nabii: ‘BWANA amekujibu nini?’ au ‘Je, BWANA amesema nini?’